MAMBO YANAYOWEZA KUATHIRI MPANGILIO WA HEDHI YAKO


HAYA NDIO MAMBO YANAYOWEZA KUATHIRI MPANGILIO WA HEDHI YAKO:👇

 
  1. Mwili kuwa msongo wa sumu nyingi, kunaweza kuathiri ukomavu wa mayai na kuathiri homoni za uzazi.
 
  2. Kuwa na kitambi na uzito mkubwa.Unapokuwa na mafuta ya ziada na sukari ya ziada isiyotumika mwilini huathiri mwili na kuvuruga homoni za uzazi, hivyo inaathiri hata utendaji wa ovari na kushindwa kukomaza mayai.
 
  3. Mwanamke kuwa na magonjwa ya tezi za shingo na tezi kwa ujumla, tezi ya thyroid ikipata shida hata ovari zinaathirika na kushindwa kukomaza mayai.
 
  4. Mlo mbovu wa chakula na vilevi, wanawake wengi hasa mjini hula vyakula ambavyo huleta changamoto kwenye afya kama vyakula vyenye sukari nyingi, mafuta mengi, pombe, sigara, shisha nk.
 
  5. Matumizi ya njia za kupanga uzazi kama sindano, vidonge, kijiti, P2, Kipandikizi n.k
 
  6. Kubadili mazingira ya kuishi/ kusafiri hasa sehemu yenye hali ya hewa tofauti na ulipokuwa unaishi awali kunaweza athiri mzunguko wa hedhi.
 
  7. Msongo wa mawazo.
 
  8. Mwanamke kusumbuliwa na maambukizi ya bakteria kama UTI, fangasi na P.I.D.
 
  9. Kufanya mazoezi magumu na kupitiliza.
 
  Ukiona unapata tatizo la hedhi muhimu kuonana na daktari kupata ushauri na tiba.
 
  Je, wewe namba ngapi inakuhusu hapa?.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.