FAHAMU KUHUSU INI?


 
🔵FAHAMU KUHUSU INI NA KAZI ZAKE na ni kwanini ni KIUNGO MUHIMU SANA MWILI.

  👉Fahamu ya kwamba Karibu kila kitu tunachokula na kunywa hupitia kwenye ini. Hata kemikali zinazogusa ngozi yetu na sumu tunayovuta hewa yake hupitia kwenye ini letu. Ini letu lina kazi nyingi muhimu za kufanya mwili mwetu ili tuendelee kufanya kazi ipasavyo. Kati ya kazi hizi muhimu moja wapo ni kuondoa sumu mwilini mwetu na kubadilisha virutubishi kwenye chakula kuwa nguvu/nishati. Hata hivyo, ini lililoharibika haliwezi kufanya kazi hizi ipasavyo, kwa hivyo ni muhimu kudumisha afya ya ini lako.
  ✅Fahamu Ukweli kuhusu INI.

👉Fahamu ya kwamba INI ni ogani kubwa zaidi ya ndani ya mwili wetu.
 
👉linapatikana upande wa kulia wa kiwiliwili chako, nyuma ya mbavu zako linaweza kujikarabati lenyewe na kutengeneza tishu mpya za ini zenye afya.
 
👉Seli za ini huvunjavunja mafuta na kutoa nguvu/nishati mwilini.
 
👉lita 1.5 za damu hupita kwenye ini lako kila dakika
 
👉Mtu yeyote anaweza kupata ugonjwa wa ini Kuna magonjwa mengi ya ini ambayo yanaweza kuathiri watu wakubwa na watoto. Watu walio katika hatari ya ini kuharibika ni pamoja na watu ambao: 👇
 
1. wana uzito kupita kiasi au wanene sana na wana ini lililojaa mafuta
   2. hunywa pombe kwa wingi
   3. Wenye maambukizi ya virusi ambayo hayajatambuliwa au kutibiwa kama vile Homa ya manjano ya B(hepatitis B) au Homa ya manjano ya C(hepatitis C). 
  4. wenye tatizo la mfumo wao wa kinga ya mwili ambalo husababisha ugonjwa wa ini
   5. waliozaliwa na ugonjwa wa ini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.