Sababu za Mwanaume Kushindwa Kumpa Mimba Mwanamke
✍🏻 Mara nyingi, mwanaume kushindwa kumpa mimba mwanamke kunatokana na matatizo ya kuzaliwa nayo kama vile:
⛔➡️ Korodani Kushindwa Kushikana Vizuri ("Undescended Test")
Hii hutokea baada ya vichocheo (hormone) kupata hitilafu na kuweza kuleta matatizo ya uzalishaji wa mbegu za kiume ambazo kitaalamu huitwa "spermatogenesis." Ingawa mrija wa kutolea mbegu unakuwepo, hakuna mbegu zinazozalishwa.
⛔➡️ Tatizo la Kimaumbile la Mrija wa Kutolea Mbegu (Hypospadias)
Katika hali hii, mrija wa kutolea mbegu pamoja na mkojo (urethra) huota sehemu ya chini ya uume, hivyo kusababisha mbegu kutoweza kufika sehemu ya ndani ya uke. Tatizo hili kitaalamu huitwa *Hypospadias*.
⛔➡️ Korodani Kupata Joto Sana (Termal Factor)
Hali hii husababisha hitilafu kwenye korodani na kufanya mbegu zisitoke zikiwa na afya nzuri. Tatizo hili huwakumba zaidi madereva wanaosafiri safari ndefu kwa zaidi ya siku mbili.
⛔➡️ Magonjwa ya Zinaa
Magonjwa ya zinaa kama yale yanayosababishwa na bakteria aina ya *Chlamydia* yanaweza kusababisha tatizo la uzazi kwa mwanaume. Pia, tatizo la tezi za shingoni (*Mumps*) linaweza kuathiri korodani na kusababisha mbegu kutozalishwa.
⛔➡️ Kuvuta Sigara na Kunywa Pombe Kupita Kiasi
Kuvuta sigara kwa wingi na kunywa pombe kupita kiasi husababisha hitilafu ya uzalishaji wa mbegu za kiume.
⛔➡️ Matatizo ya Afya kama Utapiamlo
Matatizo yanayodhoofisha mwili kama utapiamlo yanaweza pia kusababisha hitilafu ya uzalishaji wa mbegu.