Kumwaga Shahawa Zenye Damu
Kutoa shahawa zilizochanganyika na damu ni hali isiyo ya kawaida kwa mwanaume. Ingawa inaweza kutisha, mara nyingi huashiria tatizo ambalo linaweza kutibika iwapo hatua sahihi zitachukuliwa mapema.
Visababishi Vikuu vya Shahawa Zenye Damu:
- Maambukizi kwenye Korodani au Tezi Dume: Haya ni sababu kuu inayoweza kusababisha damu kujitokeza kwenye shahawa.
- Maambukizi au Michubuko katika Mrija wa Mkojo: Michubuko inaweza kusababishwa na kuumia au maambukizi makali.
- Magonjwa ya Zinaa: Magonjwa kama kisonono (Gonorrhea) yanaweza kusababisha mchanganyiko wa damu na shahawa.
- Saratani ya Tezi Dume: Wanaume walio na umri zaidi ya miaka 45 wakiwa na dalili hizi wanapaswa kuchunguzwa kwa sababu ya hatari kubwa ya saratani ya tezi dume.
Dalili za Onyo Zinazohitaji Tiba ya Haraka:
- Kuwasha au maumivu wakati wa kukojoa
- Mkojo wenye damu
- Maumivu ya chini ya mgongo au tumboni
- Uvimbe kwenye korodani
Namna ya Kudhibiti na Kutibu Tatizo:
- Kufanya vipimo vya afya mara kwa mara kwa wanaume wenye umri mkubwa ili kuchunguza hali ya tezi dume.
- Kutumia dawa zinazotolewa na daktari kwa ajili ya maambukizi ya bakteria au magonjwa ya zinaa.
- Kuepuka tabia hatarishi zinazoweza kusababisha maambukizi ya mfumo wa uzazi.
Kumbuka:
Kwa mwanaume mwenye changamoto ya kutoa mbegu chache, nyepesi, au mwenye tatizo la kuwahi kufika kileleni na kushindwa kurudia tendo la ndoa, ni vyema kutumia bidhaa za asili au ushauri wa mtaalamu ili kuboresha afya ya uzazi.